Mkutano huo unasimamiwa na Baraza la Kuleta Maelewano kati ya Madhehebu za Kiislamu, na kauli mbiu ya mwaka huu ni: "Mtume wa Rehma na Umma Mmoja."

9 Septemba 2025 - 08:55

Ripoti kwa Picha | Mkutano wa 39 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu - Tehran, Iran

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– limeripoti kuwa Mkutano wa 39 wa Kimataifa kuhusu Umoja wa Waislamu umeanza rasmi leo Jumatatu, tarehe 8 Septemba 2025, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano, Jijini Tehran - Iran.

Katika hafla ya ufunguzi, Rais wa Iran, Masoud Pezzekian, alihudhuria pamoja na wasomi na viongozi wa Kiislamu kutoka zaidi ya nchi 80 duniani, sambamba na wageni 210 wa ndani kutoka sehemu mbalimbali za Iran.

Katika mkutano huu muhimu:

  • Karatasi za kitaaluma 148 kati ya 392 zilizowasilishwa zimekubaliwa kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye kongamano hilo.

  • Mkutano huu utaendelea kwa siku tatu, kuanzia tarehe 8 hadi 10 Septemba 2025.

Mkutano huo unasimamiwa na Baraza la Kuleta Maelewano kati ya Madhehebu ya Kiislamu, na kauli mbiu ya mwaka huu ni: "Mtume wa Rehma na Umma Moja."

Ripoti kwa Picha | Mkutano wa 39 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu - Tehran, Iran

Lengo kuu la mkutano huu ni:

  • Kudumisha mshikamano wa Kiislamu

  • Kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa Kiislamu

  • Kuimarisha uhusiano baina ya Waislamu wa madhehebu tofauti

  • Kutafuta suluhisho la pamoja kwa migogoro ya kidini na kisiasa

Mkutano huu unahesabiwa kuwa jukwaa muhimu la mazungumzo ya kidini, kisiasa na kijamii, huku ujumbe wa umoja, maelewano, na haki ukisisitizwa kwa nguvu zaidi mwaka huu kutokana na hali ngumu inayowakumba Waislamu, hususan katika maeneo kama vile Palestina, Yemen na Kashmir.

Ripoti kwa Picha | Mkutano wa 39 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu - Tehran, Iran

Your Comment

You are replying to: .
captcha